Huduma zetu

Tunawahudumia watu kwa ajili ya ufalme wa Mungu kupitia huduma ama idara mbalimbali. Hata hivyo huduma zote ziko ndani ya huduma kuu nne.

wwksamaria

Wanawake Watumishi wa Kristo (WWK)

Hawa ni mama zetu, dada zetu na rafiki zetu walioungana kama kama wanawake kuitikia wito mkubwa wa kuunganisha wanawake wote wa kanisa la Samaria Spiritual Centre kumtumikia Mungu na kuifanya kazi yake kwa njia mbalimbali kanisani. Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) ushirika huu unajulikana kama “Jeshi Kubwa”

vijanasamaria

Mabalozi wa Kristo

Idara hii inahudumia vijana wa kanisani kuanzia umri wa miaka 13. Lengo kuu la idara hii ni kufundisha na kuendeleza vijana kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, na kuwaleta pamoja ili kumtumika Mungu.

cmfsamaria

Umoja wa Wanaume

Lengo kuu la ushirika huu ni kuunganisha wanaume wa kanisani kwa lengo la kumtumikia Mungu na kuwezesha kufanyika kwa kazi ya Mungu kwenye huduma mbalimbali kanisani na jamii inayotuzunguka . Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) ushirika huu unajulikana kama “Taifa kubwa”

watotosamaria

Watoto

Idara hii kiusahihi inaitwa idara ya watoto na uanafunzi. Hii ni kwa sababu inahudumia watoto wa kuanzia shule ya awali mpaka umri wa miaka 13 . Dhumuni la idara hii ni kufundisha na kuwakuza watoto kiroho na wanafunzi wazuri wa Kristo, kulingana na kitabu cha Mithali 22:6“Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.”